Alhamisi 30 Aprili 2026 - 09:30
Sheikh Ahmad Qabalan: Hatutaruhusu Lebanon kuuzwa kwa kisingizio chochote

Hawza/ Sheikh Ahmad Qabalan, amesema kuwa; kwa hali yeyote ile tunasimama na Lebanon na hatutaruhusu iuzwe kwa kisingizio chochote kile.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Sheikh Ahmad Qabalan, Mufti Ja‘fari na mwanachuoni wa Kishia wa Lebanon, katika ujumbe wake alisema: Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema katika Kitabu Chake: “Je, hujawatazama wale waliobadilisha neema ya Mwenyezi Mungu kuwa ukafiri na wakawaingiza watu wao katika nyumba ya maangamizi? Jahannam watakayoingia humo, na ni mabaya mno makaazi hayo.” Akaongeza: Mantiki ya Mwenyezi Mungu kimsingi yanaonya mataifa kwamba; hayapaswi kunyamaza mbele ya kuangamizwa kwa nchi zao au kuzitoa kama bidhaa kwa ajili ya nguvu za shari; kwa sababu anayefanya hivyo ametenda aina mbaya zaidi ya usaliti dhidi ya nchi na watu wake.

Sheikh Qabalan alisisitiza: Kusaliti maadili na misingi ya kimaadili ni hatari zaidi kuliko kitu chochote, kwa sababu ndio uti wa mgongo wa nchi na msingi wa utambulisho wake. Kwa hivyo, kwa mujibu wa mantiki ya kitaifa, haijuzu kulipa kundi lolote uwezo wa kudhuru maslahi ya mamlaka na ya taifa ya nchi yake. Muhtasari wa msimamo ni kwamba nguvu au utawala usio na ustahiki wa kitaifa, kimaadili au kisiasa, hauwezi kuaminika kuendesha nchi au kushughulikia faili lolkte la ndani au ya nje.

Aliendelea kusema: Muundo wa msimamo wa kimungu hapa unaishia kwenye ukweli wa msingi, nao ni kwamba; nchi ni mali ya maadili, misingi na dhana zinazolinda utambulisho wa kimaadili wa mwanadamu na mradi wake wa maisha ya kiraia na kijamii. Hivyo, mamlaka halali huzunguka katika mhimili wa utambulisho huu wa kimaadili na mifumo inayouhakikisha.

Sheikh Qabalan alibainisha: Mamlaka ambayo inasaliti mikataba yake na misingi ya kimaadili ya utambulisho wake huanguka, na ni lazima iondolewe; na si halali kuiwezesha. Washington,  kwa karne nyingi imekuwa ikijaribu kuunda katika nchi mbalimbali duniani makundi ya kisiasa, kiusalama, kiuchumi, kimedia na kijamii ili kwa kudhibiti nyenzo za nguvu za kisiasa, kifedha, kimedia na kijamii, zitumike kwa maslahi yake yaliyojengwa juu ya uporaji, uonevu na usaliti wa maslahi ya nchi nyingine. Lebanon bila shaka haiko nje ya mipango hii, bali kinyume chake, huenda iko katika orodha ya vipaumbele vya Washington, Tel Aviv na Ulaya, pamoja na makundi ya kikanda yanayotumikia Washington kwa upofu.

Mwanachuoni huyu wa Kishia wa Lebanon alisisitiza: Wajibu wa kimaadili na kitaifa unatueka katikati ya jukumu la kulinda utambulisho wa Lebanon; kwa kiwango cha kuhudumia maslahi ya familia ya Lebanon, si kuwa katika kuuhudumia utawala wa Kizayuni wa kigaidi. Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu (wale waliobadilisha neema ya Mwenyezi Mungu kuwa ukafiri na wakawaingiza watu wao katika nyumba ya maangamizi) inatutaka kuwa na tahadhari kali dhidi ya makundi yaliyoteka mamlaka, kwa sababu baadhi yao wanasaliti ardhi, damu, historia, kujitolea na utambulisho wa nchi na watu wao; na ni wengi kama hao katika dunia hii.

Alisema: Suala kuu kwetu ni jinsi ya kuilinda nchi na watu wetu dhidi ya usaliti na kuporomoka. Wajibu huu unahusisha tabaka zote za wananchi na nguvu zote zenye athari, kwa lengo la kulinda mikataba na maslahi ya mamlaka na ya taifa la nchi yao. Hapa ndipo mchezo wa misimamo, kauli mbiu na miradi ya udanganyifu unaanza—miradi ambayo kwa hakika inasukuma mbele usaliti wa ndani kwa ajili ya ukoloni na utawala wa kigeni.

Hatutaruhusu Lebanon kuuzwa kwa kisingizio chochote; tutalinda uamuzi wa kitaifa dhidi ya ujasiri wa kichaa

Sheikh Ahmad Qabalan alisisitiza kwamba; kilicho muhimu kwetu katikati ya hali hizi zote ni Lebanon; kwa sababu tangu siku za mwanzo za kuundwa kwa nchi ambayo kimsingi iliundwa kuhudumia maslahi ya Ulaya na Magharibi, kisha Washington na Tel Aviv, na ikawekwa katika mkondo wa miradi ya kikanda na kimataifa inayohudumia maslahi na mipango ya ubeberu wa Marekani, kwa bahati mbaya bado tunaishi katika mgogoro wa mamlaka na chaguzi zake potovu.

Hakuna kitu kilicho muhimu zaidi kuliko kuitetea Lebanon, hasa katika soko chafu la kuuza na kununua ambalo serikali zinazotegemea mashirika ya kigeni zimelifanya kuwa taaluma yao.

Aliongeza: Maslahi ya kitaifa yako wazi, na miamala ya usaliti pia iko wazi; hasa kwa kuwa makundi ya nguvu za kisiasa katika nchi hii, tangu miongo kadhaa iliyopita, yamepuuza wajibu wa mamlaka na maslahi ya taifa na kuyatoa sadaka kwa Washington, kiasi kwamba katika kipindi cha uvamizi wa Kizayuni huko Beirut, yaligeuka kuwa chombo kinachotii kabisa utawala wa Kizayuni. Lau si muqawama leo Lebanon ingekuwa koloni kamili la Kizayuni.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha